”Tunakushukuru Rais Samia kwa kutupa ndege”.YANGA.

Uongozi wa Young Africans SC unapenda kutoa shukrani kwa Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia ndege ya kusafiria kwenye mchezo wetu wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika utakaochezwa nchini Algeria dhidi ya USM Alger.